Wednesday, 23 December 2015

Tamthilia ya Siri ya Mtungi ya twaa Tuzo


Siri ya Mtungi imetunikiwa Tuzo na AfriComNet Annual Award, kwa Ubora
29 Oct 2015
SyM team Timu kutoka CCP-TCCP wakisherehekea baada ya kupokea Tuzo ya Ubora kutoka AfricComNet.
Siri ya Mtungi, Tamthilia ya Televisheni ambayo ili tayarishwa na  CCP’s Tanzania Capacity and Communication Project (TCCP), ndiyo iliyo shinda Tuzo ya AfriComNet Annual Award kwa Ubora. Hii ni katika kutambua mchango mkubwa katika sekta ya "Mawasiliano na Afya" unaotelewa kwa kiwango kikubwa na watu binafsi na taasisi mbalimali nchini, mchango ambao The AfriComNet awards inautambua. 
TCCP ili tayarisha Tamthila hii ya Siri ya Mtungi katika kampeni za kuelimisha umma juu ya kuzuia mambukizi UKIMWI,Uzazi wa mpango,na uzazi salama na afya ya mtoto. Utafiti unathibitisha kuna pengo kubwa kati ya Uwelewa na Tabia. Chanzo cha habari:http:ccp.jhu.edu




Tuesday, 22 December 2015

Mafunzo mafupi ya Uandishi wa Habari

Tutumie fursa hii kujiendeleza kimasomo katika fani.
Barua hii imetumwa na ubalozi wa Ujerumani TZ.

Dear Sir/ Madam,

my name is Ramón García Ziemsen. I am the head of the journalistic training program at Germany’s international broadcaster, Deutsche Welle.

We are looking for young people from all over the world interested in a comprehensive, exceptional quality
journalism program with an international broadcaster. Candidates should have journalism experience or be passionate about switching to journalism from technology/IT, economics or the sciences. We are looking for open-minded people full of creative ideas.

The DW editorial traineeship is paid, with a gross starting salary of approx. 1,600 Euros per month.
As full-time employees, DW trainees are automatically eligible for German public health insurance.
As our trainees move to Germany from abroad, we assist them at every step of the visa process.
The traineeship  can lead to employment in one of our departments in Bonn or Berlin.
 The program covers the range of skills a journalist of the future needs: TV moderation, multimedia storytelling,
data journalism, social media and virtual reality – in seminars, workshops and of course the DW editorial offices
and our correspondent bureaux in Washington, Moscow and Brussels. DW trainees are involved in long-term innovative, international projects and have been honored in past years with the CNN Journalism Award and the Grimme Prize.

For the bilingual DW traineeship we are looking for: 
• English native speakers with a good working knowledge of German
• German native speakers with an excellent working knowledge of English

Native speakers of any other DW program language are invited to apply as well. However, very good English skills
and basic knowledge of German is required.
The successful candidates will be based in Bonn an Berlin.
Here is a link with all the information about the traineeship:

The next traineeship starts in September 2016. Applications will be accepted via our online application system
between January 11 and February 29, 2016. Applications will not be accepted at any other time.

I would like to thank you for your cooperation.
If you have any other questions, please don´t hesitate to contact us.

Best regards
Ramón García-Ziemsen

DWA Training & Kommunikation, Journalistische Ausbildung
DEUTSCHE WELLE
T. +49.228.429-2241
F. +49.228-429-2198


Thursday, 10 December 2015

Chuo kipya cha Filamu - Dar Journalism Academy

Siku moja kwenye mwezi wa tisa 2015, nilipigiwa simu na rafiki yangu wa siku nyingi ambae niliwahi kufanya nae kazi za uandishi wa habari, alinikaribisha kwenye ofisi yake mpya, nilifika ofisini hapo, kwamshangao nilikuta zana zote za utengenezaji filamu. Nilifika chuo kipya cha uandishi habari na utengenezaji wa Filamu-DAR JOURNALISM ACADEMY...
                                                                                    Simba akiwa anatoa maelekezo... 

 Nilipata fursa ya kufanya presentation juu ya "Film script writing"

                                                                                                                                                                                                                                                                                                                               Aina za kamera...


Wanafunzi wakiwa katika mafunzo ya TV pro.

Thursday, 9 April 2015

Gilasi ya Maziwa

 Siku moja Kijana mmoja mdogo aliye kuwa akiuza bidha ndogondgo alizo zibeba mikononi mwake kwa madhumini ya kutafuta ada ya shule, alijikuta akiwa amechoka huku akiwa na njaa sana.
 Akaamua aombe chakula katika nyumba aliyokuwa ameikaribia, aka bisha hodi. Kwa mshangao mkubwa macho yake yalikutana na binti mzuri aliye fungua mlango. Kwa mshituko aliamua kuomba maji badala ya kuomba chakula.
 Lakini Binti huyo alimuangalia kijana huyo na kugundua kijana huyo alikua na njaa hivyo aliingia ndani na kutoka na kikombe kikubwa kilicho jaa maziwa na kumpa. Kijana huyo alikunywa maziwa na kumuuliza yule binti alipe kiasi gani kwa kikombe hicho cha maziwa. Binti huyo alimjibu “Mama yetu alituusia hata siku moja tusimtoze mtu malipo kwa kutoa fadhila”
Kijana huyo alimuangalia Binti huyo na kujibu “Nami nakushukuru kutoka moyoni mwangu, asante sana”.
Kijana huyo alipotoka katika nyumba hiyo, sio tu alikuwa amepata nguvu bali pia imani yake kwa Mungu na watu ilikuwa imejengeka zaidi.
 Miaka mingi ilipita, siku moja binti huyo akiwa mtu mzima alipata maradhi ambayo yalimsumbua sana kiasi cha madaktari waliokua wakimuhudumia kuamua kumpeleka katika mji mkuu ambao ulikuwa na hospitali ya rufaa kwa utafiti zaidi juu ya ugonjwa huo. Kazi hiyo akapewa daktari maalum ajulikanae kama DK. Kisaka. DK Kisaka ni mtaalam wa magonjwa yenye utata wa kutibika.
 DK Kisaka aliposikia kuna Mwanamke mgonjwa ameletwa kutoka mji aliyokulia, alijihisi kuna kitu kimemgusa, hivyo haraka alivaa vazi lake la udakitari na kuelekea sehemu alipohifadhiwa Mwanamke huyo. Alipomuona tu mama huyo alimtabua papo hapo. Dk Kisaka alimuhamisha mama huyo na kumpeleka katika chumba maalum na kuanza kumuhudumu mara moja. DK Kisaka alitumia uzoefu na ujuzi wake wote kumuhudumia Mama huyo.

Baada ya Jitihada za muda mrefu Mama huyo alipona.
 DK Kisaka aliamuru ofisi ya malipo ikadirie gharama ya matibabu ya Mama huyo na kupelekewa yeye binafsi ili aidhinishe. Baada ya kuidhinisha, DK Kisaka aliandika ujumbe mdogo pembeni ya stakabadhi hiyo na kutoa maelekezo stakabadhi hiyo ipelekwe kwa Mama huyo.
 Mama huyo alipokea stakabadhi hiyo kwa hofu kubwa akijua huenda gharama za matibabu yake yakachukuwa muda mrefu kulipa. Lakini kwa mshangao mkubwa alitafakari kwenye maneno yaliyo andikwa pembeni mwa stakabadhi hiyo na kuyasoma….. “Gharama hizi zimesha fanyiwa malipo kwa glasi moja ya Maziwa” imetiwa saini na DK Kisaka.
 Machozi ya furaha yalitiririka usoni mwake huku akimshukuru Mungu: “Eeeh Mola wangu, nakushuru sana kwani kupitia nguvu zako, Mapenzi yali safiri nakupitia mioyo ya watu na kufikia mikononi mwao.

  MSOMAJI, SASA UNA MAAMUZI: Ama kutawanya ujumbe huu ili wengi wanufaike au upuuze nakujidai hujapata hisia yoyote kupitia simulizi hii…

“Ni sanaa ya hali ya juu ya Mwalimu kuibua furaha kwa kutumia ubunifu na elimu”

– Albert Einstein

Friday, 3 October 2014


Wengi wamekuwa wakisema….sasa hivi watu wako juu, studio kibaao zimefunguliwa…
Having a studio is one thing……
 
Kuwa na studio ya audio (sauti) haina maana kuwa umefanikiwa
au umeingia ndani ya fani ya utayarishaji muziki au vipindi vya redio.

Kuna maswali ya kujiuliza kabla yakuingia studio au kutengeneza studio.

Tuesday, 18 December 2012

Sharing Experience


Uzoefu

 Director, Muongozaji ni yule ambae baada kupata maelekezo kutoka kwa Mtayarishaji na kuelewa vizuri 'Script' ya mchezo wa kuigiza au tukio la kunukuliwa katika video, yeye huchukua jukumu la kuongoza tukio zima kwa jicho la ziada. Muongozaji (Director) ndiye anae panga muelekeo na aina ya picha (Camera shots) zitakazo rekodiwa, ndiye anae ongoza waigizaji wakati gani wa kuingia au kutoka katika(Set) mandhari husika na mtazamo mzima wa mandhari na wahusika katika igizo.Muongozaji husimamia igizo/tukio kuanzia maandalizi mpaka hatua za mwisho za kilicho dhamiriwa.
 Kwa maelezo ya kina tafadhali niandikie


Wednesday, 5 December 2012



SHARING EXPERIENCE

Uzoefu

Mlolongo wa majina unaoonekana mwishoni baada ya Video au vipindi vya televisheni kuisha una ashiria  nini?

 Mtayarishaji wa kipindi(Producer): Ndiye msimamizi mkuu wa utayarishaji mzima wa kipindi,video au Filamu.Yeye ndiye muandishi au mchaguaji wa simulizi (Story)au Mada au mada ya kipindi.Mtayarishaji pia huandaa mikutano ya kujadili muonekana wa kipindi/mada, ndiye anae kadiria bajeti ya utayarishaji wa video au kipindi na kutoa maamuzi ya mwisho katika swala zima la kipindi au Filamu hiyo.
 
 Waandishi wakijadiliana kuhusu igizo kabla ya kurekodiwa. 

 
 Kimela, Martha na Abdul wakijadili "Script"

Kwa maana hiyo mtayarishaji wa kipindi ana paswa kufanya kila jitihada na kujituma kuhakikisha kipindi au filamu hiyo inakaa sawa kiufundi na yaliyomo katika kipindi.