SHARING EXPERIENCE
Uzoefu
Mlolongo wa majina unaoonekana
mwishoni baada ya Video au vipindi vya televisheni kuisha una ashiria nini?
Mtayarishaji wa kipindi(Producer): Ndiye msimamizi
mkuu wa utayarishaji mzima wa kipindi,video au Filamu.Yeye ndiye muandishi au
mchaguaji wa simulizi (Story)au Mada au mada ya kipindi.Mtayarishaji pia
huandaa mikutano ya kujadili muonekana wa kipindi/mada, ndiye anae kadiria
bajeti ya utayarishaji wa video au kipindi na kutoa maamuzi ya mwisho katika
swala zima la kipindi au Filamu hiyo.
Waandishi wakijadiliana kuhusu igizo kabla ya kurekodiwa.
Kimela, Martha na Abdul wakijadili "Script"
Kwa maana hiyo mtayarishaji wa kipindi ana paswa
kufanya kila jitihada na kujituma kuhakikisha kipindi au filamu hiyo inakaa
sawa kiufundi na yaliyomo katika kipindi.
No comments:
Post a Comment