Siku moja Kijana mmoja mdogo aliye kuwa akiuza
bidha ndogondgo alizo zibeba mikononi mwake kwa madhumini ya kutafuta ada ya
shule, alijikuta akiwa amechoka huku akiwa na njaa sana.
Akaamua aombe chakula katika nyumba aliyokuwa ameikaribia,
aka bisha hodi. Kwa mshangao mkubwa macho yake yalikutana na binti mzuri aliye
fungua mlango. Kwa mshituko aliamua kuomba maji badala ya kuomba chakula.
Lakini Binti huyo alimuangalia kijana huyo na
kugundua kijana huyo alikua na njaa hivyo aliingia ndani na kutoka na kikombe
kikubwa kilicho jaa maziwa na kumpa. Kijana huyo alikunywa maziwa na kumuuliza
yule binti alipe kiasi gani kwa kikombe hicho cha maziwa. Binti huyo alimjibu
“Mama yetu alituusia hata siku moja tusimtoze mtu malipo kwa kutoa fadhila”
Kijana huyo
alimuangalia Binti huyo na kujibu “Nami nakushukuru kutoka moyoni mwangu,
asante sana”.
Kijana huyo
alipotoka katika nyumba hiyo, sio tu alikuwa amepata nguvu bali pia imani yake
kwa Mungu na watu ilikuwa imejengeka zaidi.
Miaka mingi ilipita, siku moja binti huyo
akiwa mtu mzima alipata maradhi ambayo yalimsumbua sana kiasi cha madaktari
waliokua wakimuhudumia kuamua kumpeleka katika mji mkuu ambao ulikuwa na
hospitali ya rufaa kwa utafiti zaidi juu ya ugonjwa huo. Kazi hiyo akapewa
daktari maalum ajulikanae kama DK. Kisaka. DK Kisaka ni mtaalam wa magonjwa
yenye utata wa kutibika.
DK Kisaka aliposikia kuna Mwanamke mgonjwa
ameletwa kutoka mji aliyokulia, alijihisi kuna kitu kimemgusa, hivyo haraka
alivaa vazi lake la udakitari na kuelekea sehemu alipohifadhiwa Mwanamke huyo.
Alipomuona tu mama huyo alimtabua papo hapo. Dk Kisaka alimuhamisha mama huyo
na kumpeleka katika chumba maalum na kuanza kumuhudumu mara moja. DK Kisaka
alitumia uzoefu na ujuzi wake wote kumuhudumia Mama huyo.
Baada ya
Jitihada za muda mrefu Mama huyo alipona.
DK Kisaka aliamuru ofisi ya malipo ikadirie
gharama ya matibabu ya Mama huyo na kupelekewa yeye binafsi ili aidhinishe.
Baada ya kuidhinisha, DK Kisaka aliandika ujumbe mdogo pembeni ya stakabadhi hiyo
na kutoa maelekezo stakabadhi hiyo ipelekwe kwa Mama huyo.
Mama huyo alipokea stakabadhi hiyo kwa hofu
kubwa akijua huenda gharama za matibabu yake yakachukuwa muda mrefu kulipa.
Lakini kwa mshangao mkubwa alitafakari kwenye maneno yaliyo andikwa pembeni mwa
stakabadhi hiyo na kuyasoma….. “Gharama hizi zimesha fanyiwa malipo kwa glasi
moja ya Maziwa” imetiwa saini na DK Kisaka.
Machozi ya furaha yalitiririka usoni mwake
huku akimshukuru Mungu: “Eeeh Mola wangu, nakushuru sana kwani kupitia nguvu
zako, Mapenzi yali safiri nakupitia mioyo ya watu na kufikia mikononi mwao.
MSOMAJI,
SASA UNA MAAMUZI: Ama kutawanya ujumbe huu ili wengi wanufaike au upuuze
nakujidai hujapata hisia yoyote kupitia simulizi hii…
“Ni sanaa ya hali ya juu ya Mwalimu
kuibua furaha kwa kutumia ubunifu na elimu”
– Albert
Einstein
No comments:
Post a Comment