Thursday, 9 April 2015

Gilasi ya Maziwa

 Siku moja Kijana mmoja mdogo aliye kuwa akiuza bidha ndogondgo alizo zibeba mikononi mwake kwa madhumini ya kutafuta ada ya shule, alijikuta akiwa amechoka huku akiwa na njaa sana.
 Akaamua aombe chakula katika nyumba aliyokuwa ameikaribia, aka bisha hodi. Kwa mshangao mkubwa macho yake yalikutana na binti mzuri aliye fungua mlango. Kwa mshituko aliamua kuomba maji badala ya kuomba chakula.
 Lakini Binti huyo alimuangalia kijana huyo na kugundua kijana huyo alikua na njaa hivyo aliingia ndani na kutoka na kikombe kikubwa kilicho jaa maziwa na kumpa. Kijana huyo alikunywa maziwa na kumuuliza yule binti alipe kiasi gani kwa kikombe hicho cha maziwa. Binti huyo alimjibu “Mama yetu alituusia hata siku moja tusimtoze mtu malipo kwa kutoa fadhila”
Kijana huyo alimuangalia Binti huyo na kujibu “Nami nakushukuru kutoka moyoni mwangu, asante sana”.
Kijana huyo alipotoka katika nyumba hiyo, sio tu alikuwa amepata nguvu bali pia imani yake kwa Mungu na watu ilikuwa imejengeka zaidi.
 Miaka mingi ilipita, siku moja binti huyo akiwa mtu mzima alipata maradhi ambayo yalimsumbua sana kiasi cha madaktari waliokua wakimuhudumia kuamua kumpeleka katika mji mkuu ambao ulikuwa na hospitali ya rufaa kwa utafiti zaidi juu ya ugonjwa huo. Kazi hiyo akapewa daktari maalum ajulikanae kama DK. Kisaka. DK Kisaka ni mtaalam wa magonjwa yenye utata wa kutibika.
 DK Kisaka aliposikia kuna Mwanamke mgonjwa ameletwa kutoka mji aliyokulia, alijihisi kuna kitu kimemgusa, hivyo haraka alivaa vazi lake la udakitari na kuelekea sehemu alipohifadhiwa Mwanamke huyo. Alipomuona tu mama huyo alimtabua papo hapo. Dk Kisaka alimuhamisha mama huyo na kumpeleka katika chumba maalum na kuanza kumuhudumu mara moja. DK Kisaka alitumia uzoefu na ujuzi wake wote kumuhudumia Mama huyo.

Baada ya Jitihada za muda mrefu Mama huyo alipona.
 DK Kisaka aliamuru ofisi ya malipo ikadirie gharama ya matibabu ya Mama huyo na kupelekewa yeye binafsi ili aidhinishe. Baada ya kuidhinisha, DK Kisaka aliandika ujumbe mdogo pembeni ya stakabadhi hiyo na kutoa maelekezo stakabadhi hiyo ipelekwe kwa Mama huyo.
 Mama huyo alipokea stakabadhi hiyo kwa hofu kubwa akijua huenda gharama za matibabu yake yakachukuwa muda mrefu kulipa. Lakini kwa mshangao mkubwa alitafakari kwenye maneno yaliyo andikwa pembeni mwa stakabadhi hiyo na kuyasoma….. “Gharama hizi zimesha fanyiwa malipo kwa glasi moja ya Maziwa” imetiwa saini na DK Kisaka.
 Machozi ya furaha yalitiririka usoni mwake huku akimshukuru Mungu: “Eeeh Mola wangu, nakushuru sana kwani kupitia nguvu zako, Mapenzi yali safiri nakupitia mioyo ya watu na kufikia mikononi mwao.

  MSOMAJI, SASA UNA MAAMUZI: Ama kutawanya ujumbe huu ili wengi wanufaike au upuuze nakujidai hujapata hisia yoyote kupitia simulizi hii…

“Ni sanaa ya hali ya juu ya Mwalimu kuibua furaha kwa kutumia ubunifu na elimu”

– Albert Einstein