Tuesday, 18 December 2012

Sharing Experience


Uzoefu

 Director, Muongozaji ni yule ambae baada kupata maelekezo kutoka kwa Mtayarishaji na kuelewa vizuri 'Script' ya mchezo wa kuigiza au tukio la kunukuliwa katika video, yeye huchukua jukumu la kuongoza tukio zima kwa jicho la ziada. Muongozaji (Director) ndiye anae panga muelekeo na aina ya picha (Camera shots) zitakazo rekodiwa, ndiye anae ongoza waigizaji wakati gani wa kuingia au kutoka katika(Set) mandhari husika na mtazamo mzima wa mandhari na wahusika katika igizo.Muongozaji husimamia igizo/tukio kuanzia maandalizi mpaka hatua za mwisho za kilicho dhamiriwa.
 Kwa maelezo ya kina tafadhali niandikie


Wednesday, 5 December 2012



SHARING EXPERIENCE

Uzoefu

Mlolongo wa majina unaoonekana mwishoni baada ya Video au vipindi vya televisheni kuisha una ashiria  nini?

 Mtayarishaji wa kipindi(Producer): Ndiye msimamizi mkuu wa utayarishaji mzima wa kipindi,video au Filamu.Yeye ndiye muandishi au mchaguaji wa simulizi (Story)au Mada au mada ya kipindi.Mtayarishaji pia huandaa mikutano ya kujadili muonekana wa kipindi/mada, ndiye anae kadiria bajeti ya utayarishaji wa video au kipindi na kutoa maamuzi ya mwisho katika swala zima la kipindi au Filamu hiyo.
 
 Waandishi wakijadiliana kuhusu igizo kabla ya kurekodiwa. 

 
 Kimela, Martha na Abdul wakijadili "Script"

Kwa maana hiyo mtayarishaji wa kipindi ana paswa kufanya kila jitihada na kujituma kuhakikisha kipindi au filamu hiyo inakaa sawa kiufundi na yaliyomo katika kipindi.