Tuesday, 28 April 2009

Nuru ya Kalamu

Utangulizi

Kalamu ni neno lenye maana ya kiandikio au chombo cha kuandikia.

Nuru ni mwanga, mwanga hutokana na taa za kandili,vibatali, chemni, umeme nakadhalika. Nuru ni mwanga utokanao na chanzo ambacho si lazima kiwe taa, kwamfano mwezi hutoa nuru japo nuru hiyo pia inaweza kuitwa mwanga.Lakini nuru ni zaidi ya mwanga, kwani nuru huchukuliwa kuwa ni mwanga maalum, mwanga wenye nguvu zaidi ya mwanga.Nuru, kimatumiza inaingia upande wa hisia, yani imo katika baadhi ya mambo ambayo tunayo ndani mwetu, kando yetu lakini si rahisi kuelezeka. Hivyo. Nuru ya kalamu, kwa maana kalamu ina nuru kubwa, lakini sio ukubwa wa umbile bali ukubwa wa upeo usio na mwisho.Maandishi mengi tuyasomayo yamepitia katika kalamu. Watu husoma hadi kuhitimu katika fani mbali mbali, husoma mambo ambayo yameandikwa na wanazuoni wa kubwa na wagunduzi wa mambo.Mambo yote hayo yame andikwa kwa kutumia kalamu.Hivyo tunaweza kusema kalamu inatuonesha mengi, inatufunza mengi, kalamu ina nuru.

  Nuru ni aina ya mwanga, mwana adamu huona mambo au vitu gizani kwa kutumia mwanga, ama wa kutengeneza au wa asili.Kupitia, Maandishi mwana adamu kwa karne na karne ametoa taarifa, ameelimisha amekemea na hata kutahadharisha.Hivyo kalamu ina nuru, nuru ya ajabu isiyo onekana, kwani kupitia kalamu tunaona mengi, tunajifunza mengi.

Nuru ya kalamu

Nuru ya kalamu ni kurasa za uchambuzi wa kazi za wasanii, waandishi na wapenda maadili na lugha. 

Kama hivyo ndivyo, basi watanzania wenzangu na wapenda maadisha ya simulizi na wakaribisha katika kurasa hii tujumuike kwa pamoja katika kujadili simulizi,hadithi,video, riwaya na vingine vyote ambavyo kwa njia moja ama nyingine vitakua vimehusisha maandishi na simulizi.

Walengwa katika kurasa hizi ni wanafunzi wa sekondari, vyuo vya juu, waandishi wa Vitabu, watayarishaji wa filamu,maigizo redioni, na wadau wote wa lugha ya kiswahili hususan wapenda simulizi.

Karibuni

 Nuru ya Kalamu kama kipindi

Nuru ya kalamu ni kipindi cha televisheni. Mtiririko wa kipindi utakua katika mfumo wa mahojiano pamoja na kuonesha au kusoma kazi za wasanii au waandishi.Aidha kipindi hiki kitakua na hatua tatu kuu, nazo ni utafiti, utayarishaji na urushaji/uoneshaji.

 Kipindi cha Nuru ya Kalamu kitaoneshwa katika kituo Chochote cha televisheni kitakacho kubali kuingia mkataba na watayarishaji wa kipindi.Uoneshwaji wa kipindi utazingatia muda muufaka ambao walengwa watapata nafasi ya kukiona. Kipindi kitakua cha dakika ishirini na tano na toleo la kipindi litaoneshwa na kurudiwa japo mara moja katika kipindi cha wiki moja ili kuwapa watazamaji nafasi zaidi ya kukiona.

By: Salim Gembe

Dar es Salaam

 

 

No comments:

Post a Comment