Monday, 18 October 2010

Kwanutsu kuvamia bongo...



Kwanutsu kwa robo, muigizaji aliye jijengea umaarufu inchini Kenya, sasa aamua kubadili mtindo wa ucheshi katika televisheni na video kwa madhumini ya kujakutafuta soko la kazi zake nchini Tanzania. Wabongo kueni macho, kueni wabunifu ili mbaki juu katika soko la sanaa ya maonesho.

Thursday, 8 July 2010

Filamu Jamvini





Jee ni Video au Filamu ?

    Japo nimeazimia kuongelea juu ya swala la uwigizaji na utengenezaji wa picha naona ni vyema kwanza nikaongelea juu ya video na filamu kabla sijaingia kwa undani Juu ya swala zima la hatua za utengenezaji wa picha.Kuna mgongano mkubwa katika swala zima la lugha fasaha ya picha hizi, Wengine huita Video na wengine huita Filamu. Ukweli ni kwamba yote yana maana moja, tafauti ipo katika utayarishaji kwa kuzingatia ubora na gharama.Iwe Video au iwe Film zote hizi ni picha,picha zenye nyendo/kutembe (Motion picture au Movie).

 Watu wa makamu kidogo watakumbuka enzi zile za kununua mikanda ya picha za kawaida (still picture) mikanda hii ilikua katika mfumo wa filamu (film), kulikuwa na film zenye nembo za Olympic,Agfa,Kodak, Fuji n.k. Mikanda hii (kwa uchache wake) mingine mpaka leo inauzwa katika baadhi ya studio. Na hivyo ndivyo ilivyo katika swala la sinema pia. Mpaka leo hii mikanda(filamu) ya 16 MM, 36 MM 35MM bado ipo katika soko la sinema.  Matumizi ya Filamu ya sifika kwa ubora wake, tatizo ni gharama ya kupiga picha (kurekodi) na halafu kuhariri kwa kukata kata.Wakati mwingine inabidi pia kuhariri mkanda wa sauti peke yake na kisha kuoanisha sauti na picha kwa pamoja(synchronization). Kwa sasa tekinolojia imekua sana na filamu hizi hizi zimeboreshwa na inawezekana kurekodi picha na sauti kwa pamoja. Haya yato yahitaji muda mwingi na muda ni mali na ni ghali pia. 


Mfumo wa video hautumii film bali hutumia mikanda maalum iliyo tengenezwa kwa sumaku maalum kwahiyo Video kwa tafsiri ya harakaharaka ni: Kurekodi picha na sauti katika mkanda wenye sumaku maalum (magnetic tape).

 Kwahiyo utaona kuwa swala la gharama lina changia sana katika kufanya maamuzi ya ama kutumia filamu au video. Lakini pia mbali na gharama kuna swala zima la jinsi picha zinavyo rekodiwa katika mifumo hii miwili.

                                                         

 Kwahiyo utengenezaji wa picha za kuigiza katika mfumo wa filamu wakati mwingine inajumuisha picha na sauti kwa pamoja (sio kwa watu wengi),Lakini kwasababu ya ubora wa juu, wadau wengi wa utengenezaji wa filamu hupenda kutumia mfumo ule ule wazamani wa kutumia mikanda ya filamu ya 16mm,36mm au 35mm na kurekodi picha peke ya na sauti peke yake na halafu kuziowanisha kwa pamoja .  Kwahiyo ukilinganisha gharama za utayarishaji katika soko la sinema kwa kutumia Video na Filamu, nidhahiri kwamba utayarishaji kwa kutumia video hauna gharama sana.

 Ni imani yangu kuwa, kwa maelezo haya machache niliyo tumia kujaribu kufafanua na kutafautisha kati ya video na filamu, mtakua nanyi pia mumeelewa tafauti ya vitu hivi viwili. Na pia nidhahiri kuwa hapa Tanzania tunatumia Video kutengeneza michezo yetu ya kuingiza na sio Filamu.

Tuwasiliane kwa maoni na maswali.

  

 

Tuesday, 22 June 2010

Khadija,Irene na Paul wakisikiliza kwa makini


Watayarishaji wa Vipindi vya simulizi kutoka Radio Faraja na Radio voice of Tabora katika warsha ya kujifunza jinsi ya kuhariri simulizi zinazo tolewa na washuhuda.

Sunday, 21 February 2010

Wasanii kutoka Monduli nao wamo...



Hawa ni baadhi ya wasanii kutoka Monduli wakiwa wana rekodi mchezo wa redio studioni.Wasanii hawa ambao wamechaguliwa na Mradi wa world vision katika programu yao ARK, wanatunga michezo ya redio nakurekodi.Aidha michezo yao inalenga kuelimisha jamii ya kimasai juu ya Janga la UKIMWI. Makao makuu ya kikundi hiki ni Monduli. Michezo hii hurushwa katika redio zilizo chaguliwa na World Vision, nazo ni Radio ORS,Monduli, Boma Hai FM, Hai na Radio karagwe Bukoba.

Mafunzo ya msingi ya Uandishi na Uigizaji wa michezo ya redio kwa wasanii hawa yali fanywa na Salim Gembe.Aidha katika mafunzo hayo muwezeshaji alichagua wasanii wenye vipaji kwenye maeneo mbali mbali ya sanaa redioni na kuwapa wale wenye vipaji majukuma husika.